Sunnah imamu kusoma al-A´raaf Maghrib?

Swali: Vipi ikiwa imamu atataka kusoma Suurah al-A´raaf katika Maghrib?

Jibu: Bora ni kutofanya hivo, kwa sababu hilo linawapa uzito watu. Pengine Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivo kutokana na sababu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifupisha Maghrib.

Swali: Kwa hiyo bora ni kutofanya hivo?

Jibu: Bora ni kutofanya hivo ili asiwatie watu uzito. Haitambuliki kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikariri. Hilo limepokelewa mara moja.

Swali: Kuna sababu?

Jibu: Pengine ni kutokana na sababu.

Swali: Kwa hiyo mtu hawezi kusema kuwa katika Sunnah ni kusoma Suurah al-A´raaf katika Maghrib?

Jibu: Haliko wazi. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Sunnah yake imethibiti kufupisha katika Maghrib.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23529/حكم-قراءة-سورة-الاعراف-في-صلاة-المغرب
  • Imechapishwa: 05/02/2024