al-Haakim amesema: Abu Bakr Muhammad bin Ja´far ametukhanarisha: Nimemsikia Ibn Khuzaymah bli akiulizwa:

”Ni vipi ulipata elimu?” Akajibu: ”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Maji ya zamzam ni kwa kile ambacho mtu amekunywa kwa ajili yake.”[1]

Wakati nilipoyanywa nilimuomba Allaah elimu yenye manufaa.

[1] Ahmad (3/357) na Ibn Mâdjah (3062). al-Albaaniy amesema:

”Hadiyth ni Swahiyh, kama ilivyosemwa na maimamu wengi. Nimetaja na kuzungumzia njia zake katika ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (1123) ambapo moja wapo iko katika ”as-Swahiyhah” (883).” (Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah)

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/370)
  • Imechapishwa: 17/09/2023