Wanachuoni hawakuifikia elimu yao kupitia matamanio na matumaini. Wameifikia elimu yao kupitia mapambano na bidii. Wameitumia michana na nyusiku zao katika elimu mpaka wakakua. Baadhi ya wema wamesema kuhusu mwenendo ambao hata hivyo unaweza kutumiwa katika elimu:

“Yule ambaye mwanzo wake utakuwa wenye kuunguza basi atapata mwisho wenye kuangaza.”

Yule ambaye mwanzo wa masomo yake utakuwa ni wenye bidii atapata mwisho wenye kuangaza; atajiangazia yeye mwenyewe na kuwaangazia vilevile wengine. Ambaye amesoma wasifu na historia ya wanachuoni basi ataona kuwa walikuwa wakweli tokea mwanzo. Waliitafuta kwa bidii na wakafasiri kwa ajili ya elimu. Asiyesafiri kwa ajili ya kusoma basi hatopata vilvile wanafunzi. Kwa ajili hiyo napendekeza kusoma wasifu wa wanachuoni. Hakuna kitu kinachoshaji´isha kusoma kama kusoma wasifu wa wanachuoni na kutambua namna walivyosoma na namna walivyosubiri juu ya elimu, walivyohifadhi na mengineyo mengi.

Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (Rahimahu Allaah) aliulizwa juu ya dawa ya kuhifadhi elimu. al-Bukhaariy alikuwa akihifadhi laki ya ma-Hadiyth na kipindi hicho kulikuwa njia mbalimbali za kuhifadhi. Mtu yule akafikiri kuwa kuna kitu al-Bukhaariy anachotumia. Baadhi walikuwa wakila baadhi ya vitu ili waifanye hifdhi kuwa na nguvu. Akajibu:

“Sijaona kutokana na uzowefu wangu kitu kinachonufaisha hifdhi kama shauku ya mtu na kusoma sana.”

Ni mambo mawili:

1- Shauku ya mwanafunzi. Hivi ndivyo walivyokuwa wanachuoni. Ni lazima kuwepo shauku, utashi na kiu chenye nguvu. Utaitafuta elimu usiku na mchana. Fikira zako zote zitakuwa katika elimu.

2- Kusona sana. Usitosheke na elimu. Elimu ni mgeni wako mtukufu. Ukimkirimu, basi atabaki kwako, na ukimwacha, naye anakuacha. Kiasi ambacho utaikimbilia elimu nayo itakukimbilia. Kiasi ambacho utaghafilika nayo nayo itaghafilika na wewe na kwenda zake.

Kuhifadhi ndio msingi wa elimu. Wanachuoni walikuwa wakihifadhi. Usimjali yule anayekuzuia kuhifadhi. Kuhifadhi kunabaki na uelewa unakuja na kwenda zake. Uelewa unakuja pale ambapo hifadhi imekita na hivyo kunabaki hifadhi na uelewa vyote viwili.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Fadhwl-ul-´Ilm wa Ahlihi wa Swifatuhum http://saleh.af.org.sa/sites/default/files/101.mp3
  • Imechapishwa: 11/03/2017