Masomo ambayo mwanafunzi anayapa kipaumbele

Moja katika sifa za wanachuoni na wanafunzi ni kuwa wanatilia mkazo juu ya yale yanayowafanya kumuabudu Allaah kikweli; nayo ni Tawhiyd na ´Aqiydah sahihi. Kikubwa kinachotafutwa ni imani. Kwa ajili hiyo Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ

“… isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema.”[1]

Wanachuoni wanasema kuwa Allaah ameanza kwa elimu kwa kuwa imani ndio elimu. Ikiwa imani ndio elimu basi elimu ilio bora kabisa ni imani. Imani, wanachuoni wanasema, ni Tawhiyd na ´Aqiydah sahihi. Kwa ajili hiyo wanachuoni kutoka katika Ahl-us-Sunnah na wafuasi wa Salaf walikuwa wakiipa kipaumbele maudhui hii. Ni kosa kutoielewa na kuimairi ilihali unamairi mambo mengine ambayo hayana umuhimi sawa. Ni kasoro ukawa huwezi kuzungumzia au kuelewa vizuri jambo ambalo limefungamana na Tawhiyd au ´Aqiydah – ambayo ndio haki ya Allaah – kisha wakati huohuo ukawa unayajua mambo mengine.

Baada ya hapo wanajifunza mambo yanayoisahihisha dini yao, nayo ni ´ibaadah na elimu kuhusu ya halali na ya haramu. Mja anatakiwa ajifunze hatua kwa hatua kwa mujibu wa fadhila na uzito wa elimu. Ni kasoro akawa ni mwenye kubobea katika historia na wakati huohuo haelewi Tawhiyd, Sunnah, swalah, zakaah, swawm, hajj na mambo mengine muhimu.

[1] 103:03

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Fadhwl-ul-´Ilm wa Ahlihi wa Swifatuhum http://saleh.af.org.sa/sites/default/files/101.mp3
  • Imechapishwa: 11/03/2017