Swali: Ni ipi hukumu ya kuwalea wanyamawakali, wakiwemo simba na simbamarara, kwa njia ya kwamba wakaishi mahali pa mtu anapopumzikia wakati wa kiangazi?
Jibu: Haijuzu. Haijuzu kuwalea na kujipatishia wanyamawakali. Haijuzu. Kinachofaa ni kujipatishia mbwa kwa ajili ya lengo alilolitaja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama vile ulinzi au kukuelekeza njia.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
- Imechapishwa: 13/05/2023