Simba na simbamarara mahali pa mapumziko wakati wa kiangazi

Swali: Ni ipi hukumu ya kuwalea wanyamawakali, wakiwemo simba na simbamarara, kwa njia ya kwamba wakaishi mahali pa mtu anapopumzikia wakati wa kiangazi?

Jibu: Haijuzu. Haijuzu kuwalea na kujipatishia wanyamawakali. Haijuzu. Kinachofaa ni kujipatishia mbwa kwa ajili ya lengo alilolitaja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama vile ulinzi au kukuelekeza njia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
  • Imechapishwa: 13/05/2023