Swali: Sigara ikiwa sio chakula wala kinywaji na wala haifiki kooni inakuwa ni katika vitu vyenye kufunguza?

Jibu: Kuvuta sigara ni haramu kwako katika Ramadhaan na miezi mingine. Ni mamoja mchana au usiku. Kwa hivyo mche Allaah na akachana na uvutaji sigara kwa ajili ya kumtii Allaah. Ilinde imani yako, afya yako, mali yako na watoto wako na uchangamfu wako pamoja na familia yako ili Allaah aweze kukuneemesha kwa afya njema.

Kuhusu maneno yako kwamba sigara sio kinywaji. Mimi nakuuliza kitu: Si husemwa kuwa fulani anakunywa – يشرب – sigara au haisemwi hivo? Husemwa hivo. Unywaji unatofautiana kutegemea na kitu chenyewe. Huku ni kunywa bila ya shaka. Lakini hata hivyo ni kinywaji chenye madhara na cha haramu.

Mimi namnasihi mtu huyu na wengine mfano wake wamche Allaah juu ya nafsi zao, mali zao, watoto wao na familia zao. Mambo yote haya ya utumiaji wa sigara yanamletea madhara mwenye nayo. Kwa haya tunapata kuelewa kuwa kuvuta sigara kunamuharibia mfungaji swawm yake pamoja na madhambi yanayopatikana juu yake. Ninamuombea Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) yeye na ndugu zetu wengine atulinde kutokamana na yale yanayomghadhibisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/202-203)
  • Imechapishwa: 09/06/2017