Ahl-us-Sunnah wanaonelea kuwa utawala wa Kishari´ah unapitika kwa njia zifuatazo:
Mosi: Ah-ul-Hall wal-´Aqd kumteua kiongozi[1].
Pili: Kwa mabavu.
Yule ambaye atashinda kimabavu na akawaita watu wampe kiapo cha usikivu na utiifu, basi katika hali hiyo itakuwa ni wajibu kumtii. Vilevile akiwepo mmoja katika Ahl-ul-Hall wal-´Aqd akamteua kiongozi na wakampa kiapo cha usikivu na utiifu, basi ni wajibu kufanya hivo. Haya yamepitika katika historia ya Kiislamu. Kiapo walichopewa makhaliyfah waongofu ilikuwa kwa khiyari. Kuhusiana na kiapo cha viongozi kati ya Banuu Umayyah na Banul-´Abbaas mpaka hii leo imepitika kwa mabavu na sio kwa khiyari.
Hizo njia zote mbili ni jambo la Kishari´ah ambalo linapelekea katika hukumu za Kishari´ah; kuwatii, kutowafanyia uasi, kuwapenda, kuwanusuru katika yale ambayo Allaah (´Azza wa Jall) amewajibisha na kuamrisha kuwanusuru. Hii ni sifa wanayojipambanua nayo Ahl-us-Sunnah kutokamana na Khawaarij na watu wengine wa Bid´ah.
Leo kumetokea tofauti nyingi katika msingi mkubwa kama huu. Mwokovu ni yule aliyeokolewa na Allaah (Jalla wa ´Alaa).
Wengi ambao wanajinasibisha na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanapuuzia suala hili la uongozi. Ni lazima kwa mtu achukue ´Aqiydah yote ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah pasi na kutenganisha mlango na mwengine. Kwa sababu tukifanya hivyo basi tutakuwa ni wenye kufuata matamanio kiasi fulani. Mlango huu wanachuoni wanauita: Milango ya I´tiqaad kuhusu uongofu. Kwa sababu wametofautiana na Khawaarij, Mu´tazilah, Ashaa´irah na wengineo.
[1] Tazama https://firqatunnajia.com/ni-kina-nani-ahl-ul-hall-wal-aqd-wanaomteau-mtawala/
- Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 150-151
- Imechapishwa: 27/08/2020

Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 150-151
Imechapishwa: 27/08/2020
https://firqatunnajia.com/sifa-wanayojitofautisha-kwayo-ahl-us-sunnah-na-khawaarij/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)