Sifa tatu za kipekee kwa al-Bukhaariy


Muhammad bin Abiy Haatim amesema: Nimemsikia al-Husayn bin Muhammad as-Samarqandiy akisema:

“Katika sifa zote Muhammad bin Ismaa´iyl alikuwa akisifika kwa sifa tatu: Alikuwa ni mwenye maneno machache, alikuwa si mwenye tamaa juu ya yale yaliyoko kwa watu na alikuwa si mwenye kujishughulisha na mambo ya watu. Kujishughulisha kwake kote kulikuwa katika elimu.”

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (12/448)
  • Imechapishwa: 21/11/2020