Si sahihi kufasiri namna hiyo

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Watu aina tatu Allaah hatowatazama siku ya Qiyaamah, hatowatakasa na watakuwa na adhabu kali: mwanaume mwenye kuburuta kikoi chake, mwenye kufanya masimango kwa kile alichokitoa na yule mwenye kuuza bidhaa yake kwa kiapo cha uongo.”[1]

Je, maana ya hatowatazama ni kwamba hatowarehemu?

Jibu: Huku ni kupindisha maana. Si sahihi. Hata hivyo makusudio hapa ni kwamba amewakasirikia. Vinginevyo Yeye (Jalla wa ´Alaa) anamuona kila mtu; hakuna chochote chenye kujifcha Kwake. Lakini matamshi yanayosema:

”Allaah hatowatazama… ”

”Hatowazungumzisha… ”

yanaashiria kwamba Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) amewakasirikia. Vinginevyo haitakiwi kupindisha maana kwamba ni rehema. Hata hivyo sentesi ”Allaah hatowatazama… ” makusudio ni kwamba hatowarehemu na kwamba hatowaridhia, bali atawakasirikia kutokana na matendo yao mabaya. Hivo ndivo tamko linavyopelekea.

Swali: Kwa hivyo tamko linatakiwa kupitishwa kwa udhahiri wake?

Jibu: Ndio, kwa udhahiri wake ingawa linapelekea ghadhabu. Hatowazungumzisha, hatowatakasa na watakuwa na adhabu kali kunaashiria kwamba amewakasirikia.

[1] Muslim (406).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24076/هل-يصح-تاويل-لا-ينظر-الله-اليه-بالرحمة
  • Imechapishwa: 23/08/2024