Swali: Ni ipi adhabu ya kunywa pombe mtu anapokunywa mara ya kwanza?

Jibu: Zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakipigwa bakora arobaini. Wakati ´Umar alipoona watu wanapitiliza katika jambo hilo akafanya mijeledi themanini. Baada ya hapo Maswahabah wakaamua kufanya bakora themanini. Kisa cha ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) kinafahamisha ghera yake na kutopendelea kwake. Alipohakikisha mtoto wake amekunywa kileo hiki akamsimamishia adhabu yeye na marafiki zake. Walikuwa wameelewa makosa na kuona kwamba hakileweshi. Lakini alipouliza na akatambua kuwa kinalewesha aliwatekelezea adhabu ´Ubaydullaah bin ´Umar na marafiki zake waliokuwa pamoja naye. Kitendo hicho ni katika uangalizi wake (Radhiya Allaahu ´anh) katika kuwalinda waislamu dhidi ya shari, kufunga njia za shari na kupupia kuisalimisha jamii kutokana na maharibifu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24031/كم-حد-شارب-الخمر
  • Imechapishwa: 23/08/2024