Si ruhusa kwa mtu yeyote kukurupuka kuifasiri Qur-aan

Hakuna yeyote ambaye ana haki ya kukifasiri Kitabu cha Allaah kinyume na vile alivyokifasiri Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), walivyokifasiri Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum) au wakaafikiana juu yake waislamu. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye mjuzi zaidi wa watu juu ya tafsiri ya Kitabu cha Allaah, mtoa nasaha zaidi kwa Allaah na kwa waja Wake. Vivyo hivyo Maswahabah zake ndio wajuzi zaidi baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya tafsiri ya Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall) kama ambavo wao ndio watu wajuzi zaidi wa Sunnah na wenye kuwatakia watu mema zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (01/121)
  • Imechapishwa: 21/02/2020