Shubuha za wenye kusherehekea maulidi

Swali: Ni zipi shubuha wanazozitoa wanaosema kuwa kusherehekea maulidi ni Sunnah khaswa mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hoja yao tata ni kuiga maadui wa Allaah, kwa maana ya kuwaiga mayahudi na manaswara. Wao wanafanya hivyo, basi nao husema kwamba wanafanya kama wao. Wanasema kwa nini wasimtukuze Mtume wao kama wao wanavyotukuza? Lakini Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tayari ametukuzwa kwa yale aliyoyaweka Allaah katika Shari´ah kupitia kwake. Tunamtukuza kwa kumswalia, kufuata Sunnah yake, kushuhudia Ujumbe wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kulingania katika dini yake na kuonya dhidi ya kumpinga (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kumtukuza si kwa Bid´ah hizi na kuzua mazazi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2366/شبهة-من-يحتفلون-بالموالد-والرد-عليها
  • Imechapishwa: 09/01/2026