Swali: Ni ipi hukumu ya kusherehekea siku ya mama, siku ya mwalimu au sikukuu zengine mbali na hizo?

Jibu: Hapana. Hakuna sikukuu isipokuwa ´Iyd-ul-Fiwtr au ´Iyd-ul-Adhwhaa´. Katika Uislamu hakuna zaidi ya sikukuu hizi mbili. Haijalishi kitu kama ni siku ya taifa, siku ya mama wala siku nyengine yoyote. Haijuzu kufanya hivi. Huku ni kuzua Bid´ah ambayo haikuwekwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (58) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/15-01-1438-ighastat.mp3
  • Imechapishwa: 22/10/2017