Shaykh Swaalih al-Fawzaan akiraddi utata wa Jamaa´at-ut-Tabliygh

Swali: Ni ipi tafsiri ya Aayah:

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ

“Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa kwa watu.” (3:110)

kwa babu baadhi ya watu ambao wameunda misingi mbali mbali kwa Jamaa´at-ut-Tabliygh wanaifasiri: kutoka siku arubaini kwa mwaka?

Jibu: Ni kuibadili Qur-aan na ni tafsiri isiyohusiana chochote na hilo. Hakusema wanatoka [kharajat] kwa watu, bali Amesema: uliotolewa [ukhrijat] kwa watu.

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amewateua. Hii haina maana ya mtu kutoka siku nne au miezi kumi. Hata hivyo maana ya Aayah hii ni kwamba, Ummah huu umechaguliwa katika Ummah zingine zote kutokana na yale Allaah Aliyotaja:

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ

“Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah.” (3:110)

Hakusema kuwa wanatoka miezi mine au siku arubaini. Yote haya ni katika mabadilisho na upotevu wa Ahl-ul-Bid´ah, na kuzungumza juu ya Allaah pasi na elimu. Ni katika kufasiri Maneno ya Allaah kwa tafsiri nyingine isiyokuwa ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ”Ahmiyyat-ul-´Ilm wal-´Ulamaa’ fiy Hayaat-il-Muslimiyn”, sehemu ya 02
  • Imechapishwa: 03/09/2020