Swali: Nini maana ya Hadiyth hii, je ni sahihi:
“Atakayefunga Ramadhaan kwa imani na kutaraji malipo, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia na yatayokuja?”
Jibu: Hadiyth ni Swahiyh ameitoa al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Abu Hurayrah, lakini hakuna na “yatayokuja”. Ni kwamba atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia. Kusudio ni madhambi madogo kwa makubaliano ya wanachuoni. Ama madhambi makubwa yanahiyajia tawbah khaswa. Imeshurutishwa sharti tatu mpaka mtu awe kupata ujira huu mkubwa kusamehewa madhambi yake yaliyotangulia:
1- Sharti ya kwanza afunge Ramadhaan.
2- Sharti ya pili swawm yake iwe kwa imani ya tatu iwe swawm yake ni yenye kutaraji. Ama imani asadikishe kweli kuwa Allaah kafaradhisha juu yake swawm na afunge swawm ya ´ibaadah na si swawm ya ada na wala si swawm kama dawa ya mwili wake.
Ama kutaraji ni kwamba ataraji ujira wake kwa Allaah na hii ndio Ikhlaasw kwa Allaah (´Azza wa Jall).
- Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://alwasabi.al3ilm.com/alfatawaa
- Imechapishwa: 10/05/2020
Swali: Nini maana ya Hadiyth hii, je ni sahihi:
“Atakayefunga Ramadhaan kwa imani na kutaraji malipo, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia na yatayokuja?”
Jibu: Hadiyth ni Swahiyh ameitoa al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Abu Hurayrah, lakini hakuna na “yatayokuja”. Ni kwamba atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia. Kusudio ni madhambi madogo kwa makubaliano ya wanachuoni. Ama madhambi makubwa yanahiyajia tawbah khaswa. Imeshurutishwa sharti tatu mpaka mtu awe kupata ujira huu mkubwa kusamehewa madhambi yake yaliyotangulia:
1- Sharti ya kwanza afunge Ramadhaan.
2- Sharti ya pili swawm yake iwe kwa imani ya tatu iwe swawm yake ni yenye kutaraji. Ama imani asadikishe kweli kuwa Allaah kafaradhisha juu yake swawm na afunge swawm ya ´ibaadah na si swawm ya ada na wala si swawm kama dawa ya mwili wake.
Ama kutaraji ni kwamba ataraji ujira wake kwa Allaah na hii ndio Ikhlaasw kwa Allaah (´Azza wa Jall).
Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://alwasabi.al3ilm.com/alfatawaa
Imechapishwa: 10/05/2020
https://firqatunnajia.com/sharti-mbili-ili-mtu-swawm-yake-ya-ramadhaan-izae-matunda/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)