Swali: Ni yepi maoni yenye nguvu kuhusu kuweka shahidi wakati wa kumrejea mke. Je, inasemwa kuwa ni wajibu au inapendeza?
Jibu: Inapendeza. Ni kama mfano wa Aayah:
وَأَشْهِدُوا إِذَا تَبَايَعْتُمْ
”Lakini shuhudisheni mnapouziana.”[1]
Hili sio lazima. Ni kwa ajili ya mwongozo tu.
[1] 02:282
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (39)
- Imechapishwa: 26/05/2023