Serikali inamlazimisha kuchukua urithi wa baba yake kafiri

Swali: Baba yangu amekufa Amerika na amekufa katika dini isiyokuwa ya Kiislamu. Serikali huko ikawagawia mali warithi kwa nguvu. Je, inajuzu kwangu kuchukua mali hiyo kwa kuwa mimi ni mwanae?

Jibu: Hapana, usichukue. Sio fungu lako. Wataomrithi ni watoto wake makafiri. Mtoto wake ambaye ni muislamu hamrithi. Hana lolote kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (55) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-11-10.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020