Sehemu ya nywele zake mwanamke imeonekana wakati wa swalah

Swali: Mwanamke ameswali swalah ya faradhi na sehemu ya nywele zake ilikuwa wazi pasi na yeye kujua. Mume wake akamzindua baada ya yeye kumaliza kuswali. Je, ni lazima kuirudia?

Jibu: Swalah yake ni sahihi muda wa kuwa hakujua mpaka alipomaliza kuswali. Swalah yake ni sahihi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (44)
  • Imechapishwa: 12/07/2024