Wewe na mali yako ni milki ya baba yako, na si mama yako

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wewe na mali yako ni milki ya baba yako.”[1]

Je, anaingia pia mama?

Jibu: Udhahiri, hapana. Ni jambo maalum kwa baba. Hata hivyo ni vyema akimpa kwa ajili ya kumtedea wema na ihsani mama na kumridhisha.

[1] Abu Daawuud (3530), Ibn Maajah (2292) na Ahmad (7001). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (1870).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (44)
  • Imechapishwa: 12/07/2024