Swali: Ni ipi hukumu ya kuwatolea salamu Ahl-ul-Bid´ah, kukaa nao na kutembea nao?

Jibu: Ni wajibu kuwasusa Ahl-ul-Bid´ah. Ikiwa hawakutubu baada ya kuwanasihi haijuzu kukaa nao ili asije kumuathiri. Ni wajibu kuwasusa.

Lakini hata hivyo ni lazima tujue ni nini Bid´ah. Baadhi ya watu hawajui Bid´ah ni kitu gani. Kila mwenye kutofautiana naye au kutokubali maoni yake anamfanyia Tabdiy´. Sivyo hivyo. Bid´ah imebainishwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa salla) pale aliposema:

“Atakayezusha katika dini yetu hii yasiyokuwemo atarudishiwa mwenyewe.”

“Tahadharini na mambo ya kuzua. Hakika kila kitakachozushwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”

Bid´ah ni kile chenye kwenda kinyume na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13385
  • Imechapishwa: 24/06/2020