Swali: Mtu ambaye shaytwaan amemshawishi na akamwende mwanamke ambaye ni ajinabi na mapenzi bila ya jimaa kitendo hicho kitahitajia adhabu kama adhabu ya kufanya zinaa au inatosheleza kuomba msamaha?

Jibu: Tawbah na kuomba msamaha kunatosheleza. Vilevile ahifadhi swalah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alijiwa na mtu ambaye alikuwa amefanya kila kitu na mwanamke mmoja isipokuwa jimaa tu, mtu huyu akaja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumuuliza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akakaa kimywa mpaka kulipoteremsha Kauli Yake (Ta´ala):

وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ

“Simamisha swalah katika ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku; hakika mema yanaondosha mabaya. Hivyo ni ukumbusho kwa wanaokumbuka.” (11:114)

Mtu yule akamuuliza: “Ee Mtume wa Allaah! Aayah hii inanihusu mimi mwenyewe au watu wote?” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akajibu na kusema:

“Ni kwa watu wote.”

Mwenye kuhifadhi swalah za faradhi Allaah kwa swalah hizo anamsamehe madhambi madogo madogo – himdi zote anastahiki Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13382
  • Imechapishwa: 24/06/2020