Ndugu! Tunaona watu wengi wanapoanza wanajifanya ni watu wa Ikhlaasw. Baada ya hapo kupitia matendo na maneno yake inakudhihirikia yenye kwenda kinyume na Da´wah yake. Tamahaki utamuona ameiuza dini yake. Wema na uongofu aliyokuwemo jana anayauzulu kwa ajili ya dunia. Jana ulikuwa humuoni isipokuwa na watu wa haki na uongofu, Ahl-us-Sunnah wal-Hadiyth. Lakini hii leo unamuona amebadilisha na kugeuza mambo yote. Ghafla wamuona amekuwa kinyume na ile hali yake ya kwanza. Baada ya kuwa na wanachuoni wa Sunnah na Athar, ghafla wamuona amekuwa nyuma ya dunia. Unamuona anatembea na fulani na fulani miongoni mwa watu amabo tunawajua kuwa na u-Hizbiyyah na Bid´ah. Afadhali angelikomeka hapa tu. Bali baada ya hapo anavuka na kutafuta hoja ya matendo yake. Hatimaye wamuona aanza kuwaponda wanachuoni wa Sunnah na Hadiyth, ambao walikuwa ni waalimu zake jana. Haya anayafanya pale ambapo ameshapata yale anayoyataka kwa watu wale alioungana nao. Hivi sasa ameshaipata dunia. Jana alikuwa ni mtu asiyekuwa na maana yoyote, lakini hii leo amekuwa na gari kubwa na nguvu. Amepata dunia kwa kuiuza dini yake; kwa kuacha Sunnah na Ahl-us-Sunnah na kujiunga na Bid´ah na Ahl-ul-Bid´ah.
Halafu utamuona anaanza kujitolea nyudhuru za ki-Ibliys. Ghafla utamsikia akisema ´watu hawa wana msimamo mkali`, ´hawa wana uchupaji wa mipaka`, ´hawa kazi yao ni kuwaponda wengine`, ´hawa wanatofautiana na wengine`. Matokeo yake huyu anakuwa mpinzani mkubwa wa Sunnah na Ahl-us-Sunnah na mzushi wa asli. Sisemi haya kwa kubahatisha, bali ndio uhalisia wa mambo yenyewe. Tumeshuhudia yote haya.
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=5503
- Imechapishwa: 27/08/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
Hawa ndio sababu ya vijana Salafiyyuun ulimwenguni kugawanyika
Unatakiwa kutangaza sababu za mgawanyiko wa vijana wa Salafiyyuun na wale waliosababisha hilo ili baada ya hapo uweze kufikisha haki na kuwatunza wale ambao wamewaganya vijana na kuzusha kanuni zisizokuwa za salama ili kuwatetea Ahl-ul-Dhwalaal wal-Bid´ah. Kukosoa kanuni zao zisizokuwa za salama na misingi, mifumo ya kipotevu, kuwatetea Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal,…
In "Rabiy´ al-Madkhaliy kuhusu ´Ar´uur"
Vitabu tunavyopendekeza na vitabu tunavyotahadharisha
Swali: Ni vitabu vipi unavyopendekeza na ni vitabu vipi unavyotahadharisha? Jibu: Napendekeza Qur-aan, Sunnah na vitabu vyote vya Salaf, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kwa jumla. Havihesabiki. Atakayevifanya ni vyanzo juu ya dini na elimu yake atatosheka navyo. Hahitajii vitabu vya Ahl-ul-Bid´ah. Tunatahadharisha vitabu vya Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal; vitabu vya Suufiyyah, vitabu vya Khawaarij,…
In "1. Mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah"
Tunawatahadharisha vijana wa ki-Salafiy na Ahl-ul-Bid´ah
Hii leo kuna mifano mingi katika watu mnaowajua waliokuwa wakifuata mfumo wa Salaf. Pindi walipoanza kuchanganyikana na Ahl-ul-Bid´ah wakapotea. Kwa sababu Ahl-ul-Bid´ah hii leo wana mbinu nyingi, nishati kwelikweli na mifumo - kuna uwezekano ndio mifumo iliyokuwa ikitambuliwa na mashaytwaan hapo kitambo - na wao hivi sasa wakazijua mbinu hizi,…
In "Rabiy´ al-Madkhaliy kuhusu sifa na alama za Ahl-ul-Bid´ah"