Pengine mtu akauliza kama ni wajibu kunyamaza katika Khutbah ya ijumaa ambapo Ahl-us-Sunnah wanatukanywa. Hapana, sio wajibu kunyamaza. Chukua na usoma Qur-aan. Zungumza na rafiki yako juu ya suala la kielimu. Kwa sababu Allaah (´Azza wa Jalla) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ

“Enyi mlioamini! Inaponadiwa [adhana ya] swalah siku ya ijumaa, kimbilieni katika ukumbusho wa Allaah.” (62:09)

Hakusema kimbilieni katika kutukanywa kwa waislamu. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Kumtukana Uislamu ni dhambi kubwa na kumuua ni kufuru.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema pia:

“Yule mwenye kulaani hatoshuhudilia na wala hatoombea.”

Haitakikani kunyamaza kwa Khutbah kama hizi. Ninashangazwa kuona ndugu Qatar wanaenda kwa at-Twahhaan.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Naswaaih wa Fadhwaaih, uk. 273
  • Imechapishwa: 28/07/2020