Swali: Baadhi ya watu wanapoamrishwa kusoma vitabu vya Tawhiyd wanasema ´Sisi hivi tuna haja [ya kujua] mambo ya kisasa (Fiqh-ul-Waaqiy´). Kuhusu Tawhiyd inajulikana`. Ni yapi maoni yako kuhusu maneno haya?`

Jibu: Haya ni maneno batili. Haya ni maneno batili. Tawhiyd inajulikana! Ni nani amekwambia hivi? Watu wengi leo wametumbukia kwenye Shirki kubwa. Shirki ipo leo; kuna makaburi ambayo leo yanaabudiwa badala ya Allaah, yanachinjiwa na kuwekewa nadhiri katika miji mingi. Kuna watu wengi wasiojua Tawhiyd. Ashaa´irah, Mu´tazilah, Jahmiyyah, Suufiyyah, watu wa Wahdat-ul-Wujuud wanapatikana leo. Ni lazima kwa mtu ajifunze Dini yake na aielewe.

Kuhusu Fiqh-ul-Waaqiy´ nini itachosaidia ikiwa mtu sio mpwekeshaji. Mpwekeshaji ndio mwenye kufahamu Fiqh-ul-Waaqiy´. Ukijifunza Dini yako na ukaisoma na ukasoma ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ndio utakuwa umefahamu mambo ya kisasa. Utajua mambo ya kisasa, ni wepi wapwekeshaji, ni wepi washirikina, utajua kuwa madhehebu ya Suufiyyah ni batili, madhehebu ya Jahmiyyah ni ya kuziharibu Sifa na Majina ya Allaah na madhehebu ya Mu´tazilah ni batili. Tawhiyd inalingania katika haya. Ama asiyeijua Tawhiyd hajui Fiqh-ul-Waaqiy´. Hivyo, haya ni maneno batili. Mpwekeshaji ndio anayejua Fiqh-ul-Waaqiy´. Asiyejua Tawhiyd hajui Fiqh-ul-Waaqiy´. Bali anakuwa ni mjinga juu ya mambo haya.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4743
  • Imechapishwa: 01/05/2015