Swali: Kuko ambao wanasema kuwa mfumo na ´Aqiydah yao ni Salafiyyah na njia yao ni Ikhwaaniyyah. Unasemaje kuhusu maneno haya?

Jibu: Tunatarajia wanatamka kweli pindi wanaposema kuwa Da´wah yao ni Salafiyyah. Je, umeona kuwa wanamwabudu Allaah kwa Salafiyyah na wanaamini yale ambayo Salaf-us-Swaalih waliyokuwa wakiamini? Ni maneno tu bila ya maana.

Imejulikana sasa kwamba ulinganizi wa kweli ni ulinganizi wa Salafiyyah. Wamepanda kwenye treni hii na wanajificha nyuma yake. Haiwezekani kabisa kufanya Salafiyyah na Ikhwaaniyyah vikawa na umoja. Ima mtu ataegemea katika upande mmoja.

Mara nyingi tumesema kuwa Da´wah ya al-Ikhwaan al-Muslimuun imejengeka juu ya kusanya kisha ndio ufundishe pasina mafundisho yoyote. Andika hilo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (600)
  • Imechapishwa: 22/04/2015