Ni lazima kuwa na elimu ya Tawhiyd kabla ya kutoka kwenda katika Jihaad?

Swali: Mimi kama kijana wa Kiislamu natakiwa kwanza kujiandaa kwa elimu, Fiqh, Hadiyth na Qur-aan halafu ndio nitoke niende katika Jihaad au naweza nikaenda hivi sasa?

Jibu: Kwanza nitaanza kwa kukujibu vile nitakavyo na halafu ndio nikujibu vile utakavyo.

Umelazimika kuufahamu Uislamu, lakini si kwa ufafanuzi wote na matawi. Kwanza unatakiwa kuisahihisha ´Aqiydah yako na ´ibaadah yako ambayo ni wajibu juu yako. Kwa kuzingatia kuwa wewe bado ni kijana, kwa mfano hauko tajiri ili ikuwajibikie kwako zakaah na kwenda kuhiji katika nyumba ya Allaah tukufu. Vijana wengi wanaishi kama jinsi tulivyosema kwa baba zao. Nitakachokusema kwa mfano huu, pasina kujali kama hili litakuwa ni kweli kwako au si kweli, haikuwajibikii kwako kuwa na elimu kuhusu zakaah ikiwa huna pesa za zakaah. Huna pesa za kwenda Hajj katika nyumba ya Allaah tukufu na kwa ajili hiyo haikuwajibikii kwako kuwa na elimu kuhusu Hajj. Hata hivyo ni wajibu juu yako kuswali na kufunga. Na kabla ya hayo ni wajibu kwako kuwa na elimu kuhusu jambo ambalo karibuni tumelitaja kwa kifupi sana, nalo ni “hapana mungu anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Mtume wa Allaah”. Neno lote hili maana yake ni nini? Kabla ya kutoka kwenda katika Jihaad, ni wajibu juu yako kwanza kumaliza wajibu huu wa kwanza. Huu ndio wajibu wako. Hivi ndivo ilikuwa kama vile ninavyotaka.

Kuhusiana na vile unavyotaka wewe, ninakwambia toka wende ukapigane Jihaad katika njia ya Allaah kama jinsi ulivo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (424)
  • Imechapishwa: 22/04/2015