Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye anadai kuwa yeye anazifahamu Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa ufahamu usiyokuwa wa Salaf?

Jibu: Ni kosa. Hapana shaka yoyote kwamba wema wetu waliotangulia ambao wameyasikia maandiko ya Qur-aan na Sunnah ni wajuzi zaidi wa tafsiri yake kuliko sisi. Huenda baadhi ya wasikilizaji au baadhi ya waliokuja nyuma wakafahamu kitu vyema zaidi, kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Huenda mfikishaji ana uelewa mzuri zaidi kuliko msikilizaji.”

Lakini kwa ujumla ufahamu wa Salaf ni mkubwa zaidi kuliko ufahamu wetu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/عليكم-بسنتي-وسنة-الخلفاء-الراشدين
  • Imechapishwa: 20/06/2022