Swali: Muislamu aseme nini wakati anapowaingilia mayahudi na manaswara kazini na ajiepushe na kuwasilimia? Vipi kumraddi mwenye kusema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimtembelea myahudi ambaye mtoto wake alikuwa mgonjwa mpaka mwishoni akasilimu. Ikiwa wao wanatupongeza kwa sikukuu zetu sisi pia tunaweza kuwapongeza kwa sikukuu zao?

Jibu: Akiingia kwenye kikao ambacho kuko waislamu na makafiri, toa salamu kwa nia ya wewe kuwasalimia waislamu. Ama ukiingia kwenye kikao ambacho hakuna muislamu hata mmoja, usiwatolee salamu.

Hata hivyo ikiwa utawaambia “Vipi hali zenu” na mfano wa hayo ni sawa. Hili halina neno kwa kuwa unamuuliza hali yake na si kwamba unamuombea du´aa. Usimuombee du´aa. Kuhusu salamu usimtolee salamu:

“Msianze kuwatolea mayahudi na manaswara salamu.”

Ni wajibu hili likatambulika.

Kuhusu kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwatembelea makafiri ili kuwalingania, wakati alipomtembelea myahudi kwa ajili ya kumlingania, haikusemwa kuwa aliwatolea salamu. Hili halikuthibiti. Aliwaeleza Uislamu na miongoni mwao kuko waliosilimu na wengine wakakataa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1430-7-20.mp3
  • Imechapishwa: 19/04/2015