Sahihi kusema “Ninayemfanya kuwa katikati ni Allaah”?

Swali: Ni upi usahihi wa ibara hii:

“Ninayemfanya kuwa katikati ni Allaah”

wakati mtu anapoulizwa ni nani anayemweka kati na kati sehemu zote?

Jibu: Ikiwa anakusudia utegemezi, basi amekosea ibara. Lakini maana ni sahihi. Lakini anatakiwa asitumii msemo huu. Kwa sababu inamfanya mtu kufahamu kuwa Allaah anamkalia kati na kati mwingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 76-77
  • Imechapishwa: 30/08/2018