Swali: Baadhi ya watu wanaenda nchikavu kabla ya swalah ya ijumaa. Je, ni wajibu kwao kurudi na kuhudhuria swalah ya ijumaa?

Jibu: Haijuzu kwao kuanza safari baada ya imamu kuadhini adhaana ya pili. Ni wajibu kwao kusimama na kuswali. Hata hivyo inafaa kwao kuanza safari kabla ya kuadhiniwa adhaana ya pili. Lakini wasiache swalah ya ijumaa. Ikiwa inaswaliwa njiani, waswali ili wapate ujira.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (13) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdah%20Fiqh-26-10-1434.mp3
  • Imechapishwa: 21/10/2017