Swali: Watu wengi wanaijua Njia iliyonyooka, lakini hawaishiki kwa uthabiti. Ni sababu zipi zinazowazuia kuishika? Ni njia zipi za tiba zitakazowafanya waifuate Njia hii iliyonyooka?

Jibu: Sababu ni nyingi. Kuacha kushikamana na haki kuna visababishi vingi. Wakati mwingine mtu huwa ni mjinga asiyejua haki. Wakati mwingine anakuwa anaijua haki, lakini matamanio yake yanambeba kwa sababu haki haiendani na matamanio yake na hivyo matamanio humpelekea kuiacha haki. Wakati mwingine humuasi Allaah kwa ajili ya kuwafurahisha jamaa zake au marafiki zake na huwapendelea kwa kutozitaka nyoyo zao zikunjike akifuata haki. Matokeo yake huwafanyia upendeleo, hunywa pamoja nao pombe na humuasi Mola wake katika kukata udugu, katika uasi kwa wazazi na katika mambo mengine kwa ajili ya kuwafurahisha jamaa au marafiki zake au mfano wa hayo. Wakati mwingine humuasi Allaah kwa ajili ya mali anayopewa na wakati mwingine kwa ajili ya kazi au cheo. Sababu zake ni nyingi. Tunamuomba Allaah atukinge.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2434/اسباب-ترك-الحق
  • Imechapishwa: 29/03/2026