Swali: Ni maoni yepi yenye nguvu juu ya saa ambayo mtu anajibiwa siku ya ijumaa? Je, ni pale ambapo imamu anaketi chini kati ya Khutbah mbili au ni ule wakati wa jioni?

Jibu: Haafidhw Ibn Hajar katika “Fath-ul-Baariy” amesema:

“Wanachuoni wametofautiana juu ya maoni arobaini. Maoni mawili ndio yenye nguvu zaidi:

1- Ni pale ambapo imamu anaketi chini mpaka kukimiwe swalah ambapo mtu anatakiwa kuomba du´aa kati ya Khutbah mbili na kwenye Sujuud ndani ya swalah.

2- Zile saa za mwisho baada ya ´Aswr.”

Maoni yaliyo na nguvu zaidi katika hayo mawili ni zile saa za mwisho baada ya ´Aswr.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14)
  • Imechapishwa: 07/06/2020