Swali: Vipi kuhusu kupiga risasi harusini?

Jibu: Hapana vibaya ikiwa ni kwa ajili ya mafunzo. Isiwe kwa ajili ya mchezo. [Ni sawa] ikiwa ni kwa ajili ya mafunzo na mazoezi.

Swali: Wanapiga milio ya risasi katika usiku wa ndoa?

Jibu: Hapana vibaya ikiwa ni kwa ajili ya mafunzo ya kulenga shabaha. Hata hivyo haifai ikiwa ni kupoteza mali tu bila faida yoyote.

Swali: Wanafanya kuwa ni kutangaza furaha ya ndoa ambapo wanapiga risasi kadhaa?

Jibu: Baadhi ya watu katika baadhi ya nchi za kusini wanaweza kufanya mambo kama hayo. Hata hivyo sasa nimefikiwa na khabari kutoka kwa baadhi ya watu kwamba wakati mwingine kunatokea maovu na mauaji. Mlenga shabaha anaweza kukosea na hivyo kukatokea mauaji. Ikiwa kunatokea maovu basi ni lazima kuyazuia. Ni lazima kwa watawala kuyazuia ikiwa ni katika mji ambapo kunakhofiwa kutokea maovu. Lakini hapana neno ikiwa ni kwa ajili ya mafunzo kama walivofanya Wahabeshi ambapo walikuwa wakijifunza kwa panga, mikuki na kurusha mishale hewani bila ya kumdhuru yeyote. Hata hivyo ni lazima kwa watawala kuyazuia ikiwa kunakhofiwa juu yake madhara popote walipo muda wa kuwa kitendo hicho kina madhara  kwa yeyote.

Mwanafunzi: Katika baadhi ya ndoa wanarusha ndege?

Ibn Baaz: Kwa sababu gani?

Mwanafunzi: Wanarusha ndege mbele ya wanawake; njiwa na shomoro?

Ibn Baaz: Bora ni kuacha kufanya hivo. Hili ni jambo jipya. Pengine ni kujifananisha na baadhi ya makafiri.

Mwanafunzi: Udhahiri wa mambo ni hivo.

Ibn Baaz: Inatakikana kuacha jambo hilo. Ni wajibu kuacha ikiwa ndani yake kuna kujifananisha. Sherehe yenyewe ni kutangaza. Kufanyika sherehe na karamu ya ndoa kunatosha kuitangaza ndoa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23917/حكم-اطلاق-النار-والطيور-اعلانا-للفرح
  • Imechapishwa: 05/06/2024