Swali: Je, afanye Rak´ah nyingi au arefushe Sujuud?
Jibu: Udhahiri wa Hadiyth unapelekea Rak´ah nyingi. Baadhi ya wanazuoni wamefadhilisha urefu wa kisimamo. Jengine ni kwa sababu katika baadhi ya nyusiku alirefusha swalah yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini bora iwe kati kwa kati; swalah yake iwe kati kwa kati, Rukuu´ yake, Sujuud yake na kisimamo chake vikaribiane ili asijifanyie uzito nafsi yake na akithirishe Rak´ah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21466/هل-كثرة-الركعات-افضل-ام-طول-السجود
- Imechapishwa: 13/04/2023