Dr Ibraahiym [ar-Ruhayliy] amesema:

”Radd inatakiwa iwe yenye kutoka kwa mwanachuoni ambaye amebobea katika elimu. Anatakiwa awe na ujuzi kwa njia iliyopambanuka kuhusu suala hilo linalofungamana na Radd kwa upande wa dalili ya ki-Shari´ah, maneno ya wanazuoni juu yake, upindaji wa ile haki kwa yule mwenye kwenda kinyume, chimbuko la utata wake, Radd ya wanazuoni juu ya utata huo na mafunzo ya maneno yao juu ya mada hiyo.”

Natamani Radd itoke kwa mwanachuoni ambaye amebobea akiwa na sifa kama ulizotaja. Hata hivyo sio lazima sifa hizi zitimie kwa kila mwenye kuraddi na si lazima azitimize sifa hizi. Endapo tutashurutisha hilo kwa kila mwenye kuraddi na kila Radd basi kungelieneza ufisadi na zingeliteka takriban ummah mzima.

Kitu ambacho kinatili nguvu kuwa sharti hizi si sahihi ni kuwa hutowapata wanazuoni Salafiyyuun wenye elimu iliobobea katika nchi nyingi za kiislamu. Hata hivyo wapo wanafunzi. Allaah amenufaisha kupitia wao pale wanapoeneza Tawhiyd na kuraddi shirki, Bid´ah na mambo ya ukhurafi.

 Napenda kumuuliza Dr Ibraahiym swali lifuatalo: Ikiwa kuna nchi ambayo kunaenea Bid´ah na maovu na wakati huohuo kukawa hakuna mwanachuoni ambaye ametimiza sharti hizo, lakini kukawepo wanafunzi waliosoma ”al-Usuwl ath-Thalaathah”, ”Kashf-ush-Shubuhaat” na ”Kitaab-ut-Tawhiyd” vya Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, ”al-Waasitwiyyah” na ”al-Hamawiyyah”  vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, ”´Umdat-ul-Ahkaam”  cha Imaam ´Abdul-Ghaniy al-Maqdisiy au  ”Buluugh-ul-Maraam” cha Haafidhw Ibn Hajar na wakati huohuo nchini mwao kukawa kumeenea kukanushwa sifa za Allaah na Bid´ah za Qadariyyah, Bid´ah za Murji-ah, waabudia makaburi na Bid´ah nyinginezo na unywaji pombe au manyanyaso kwa wanawake – ni lazima wakemee maovu haya kutokana na elimu yao au itawalazimu kunyamaza kwa sababu wao sio wanazuoni waliobobea katika elimu? Nafikiri kuwa jibu la Dr Ibraahiym ni kwamba ni lazima kwa wanafunzi hawa kuzuia maovu haya kwa kiasi cha elimu na uwezo wao kwa ajili ya kutendea kazi maneno Yake Allaah (Ta´ala):

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚوَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Wawepo kutoka kwenu watu wanaolingania kheri na kuamrisha mema na unaokataza maovu. Hao ndio waliofaulu.”[1]

Vilevile kwa ajili ya kutendea kazi maneno yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule miongoni mwenu atakayeona maovu basi ayazuie kwa mkono wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa mdomo wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa moyo wake na hiyo ni imani dhaifu mno.”[2]

[1] 03:104

[2] Ahmad (3/10) na Muslim (49).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan maa fiy Naswiyhati Ibraahiym ar-Ruhayliy min al-Khalal wal-Ikhlaal, uk. 49
  • Imechapishwa: 10/12/2022