Radd kwa anayezusha kuondoa uchawi kwa kutumia uchawi mwingine

Swali: Kuna fatwa iliyoenea ya baadhi ya wanazuoni waliohai na waliokufa (Rahimahumu Allaah) ambao wamejuzisha kuondoa uchawi kwa kutumia uchawi mwingine kutokana na dharurah. Je, haitoshi ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Adhabu ya mchawi ni kupingwa kwa upanga”?

Jibu: Kwa hali yoyote ni kwamba maoni ya pili ni kosa. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:

”Adhabu ya mchawi ni kupingwa kwa upanga”?

Ni maneno ya Swahabah hata hivyo yanayo hukumu moja kama maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Qur-aan imetaja wazi ya kwamba mchawi ni kafiri:

وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ

“Na [hao Malaika wawili] hawamfundishi yeyote mpaka wamueleze: “Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru [kwa kufanya uchawi]”.”[1]

[1] 02:102

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24603/الرد-على-من-اباح-النشرة-بالسحر-للضرورة
  • Imechapishwa: 09/11/2024