Radd kwa anayepinga kuwaozesha wasichana wadogo

Swali: Maneno ya Allaah (Ta´ala):

“… pamoja na ambao hawapati hedhi… ” (65:05)

Katika Aayah hii kunachukuliwa dalili Radd kwa wale wanaopinga kuwaozesha wasichana wadogo?

Jibu: Ndio. Ni wale ambao hawajapata hedhi kwa sababu ya utoto. Hii ni Radd ya wazi. Ni nani anayepinga kuwaozesha wasichana wadogo? Anapinga hukumu za Allaah kwa matamanio au kwa ujinga? Haijuzu kufanya hivi. Huu ni upotevu na tunaomba kinga kwa Allaah. Ni nani anayepinga kuwaozesha wasichana wadogo? Anapinga hukumu ya Kishari´ah? Dalili yake ni ipi juu ya hili? Hana dalili juu ya hili. Je, yeye ana huruma sana kwake zaidi kuliko baba yake aliyemuozesha?

Hata hivyo ikiwa baba yake amemuozesha kwa nguvu inatakiwa kumkataza ingawa hili haliwi mara nyingi. Ama kupinga kuoa wasichana wadogo moja kwa moja, huku ni kuzipinga hukumu za Allaah na wala haijuzu kufanya hivi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–15041434.mp3
  • Imechapishwa: 20/09/2020