Baba wa mume ni Mahram kwa mama wa mke?

Swali: Mwanaume atapooa mwanamke baba wa mume ni Mahram kwa mama yake na mke?

Jibu: Hapana. Baba wa mume sio Mahram kwa mama wa mke. Mke wa mtoto wake ndio atakuwa Mahram wake.

“… [pia mmeharamishiwa] wake wa watoto wenu… “ (04:23)

Ama mama yake [mke] yuko mbali na baba wa mume. Yeye ni ajinabi. Vilevile mama wa mke anakuwa ni Mahram wa mume wa msichana wake. Anakuwa ni Mahram wa mume wa msichana wake.

“… na mama wa wake zenu.” (04:23)

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com