Radd juu ya utata unaotumiwa na waabudu makaburi wengi

Swali: Katika baadhi ya njia za mawasiliano kumejitokeza mtu anayesema kuwa inajuzu kuweka kaburi kwenye msikiti kwa kutumia dalili maneno Yake (Ta´ala) katika Suurat-ul-Kahf:

قَالَ الَّذِينَ غَلَبُوا عَلَىٰ أَمْرِهِمْ لَنَتَّخِذَنَّ عَلَيْهِم مَّسْجِدًا

“Wakasema wale walioshinda katika shauri lao: “Bila shaka tutajenga msikiti juu yao.” (18:21)

Vipi kumraddi?

Jibu: Aayah yenyewe inamraddi:

قَالَ الَّذِينَ غَلَبُوا عَلَىٰ أَمْرِهِمْ

“Wakasema wale walioshinda katika shauri lao… “

bi maana hawakukubali nasaha na wakaendelea kujenga juu yao. Hii ni kwa njia ya kuwakemea. Maneno Yake:

قَالَ الَّذِينَ غَلَبُوا عَلَىٰ أَمْرِهِمْ

“Wakasema wale walioshinda katika shauri lao… “

ni kwa njia ya kuwakemea na kwamba walifanya kwa maoni yao na hawakukubali nasaha. Huyu mwenye kusema kuwa inajuzu kuweka kaburi kwenye msikiti ni mwenye kumpinga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume amemlaani mwenye kufanya hivi na akatahadharisha juu ya hili. Huyu ni mkaidi na anampinga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni mlinganizi anayelingania katika shirki. Tunaomba Allaah atulinde.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-10-30.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020