Jipime maarifa yako kuhusu swawm

Chemsha Bongo ya Ramadhaan 07

15:00

Ni zipi katika hizi alama za kubaleghe kwa mtoto?

  • Kuota nywele sehemu za siri, kumwaga manii kwa kuota, kufikisha miaka 15, kupata hedhi
  • Kuwa na busara, kuwa na mawazo mapana na sauti kubwa

Mswaliji asome duaa ya kufungulia swalah kila baada ya Rakah mbili za Tarawiyh?

  • Ndio, ni lazima
  • Inafaa, ijapo inatosha kusoma pale mwanzo wa swalah tu

Je, inafaa kutumia vyombo vya kisasa (kama vile darubini) katika kutafuta mwezi mwandamo?

  • Ni kujifananisha na makafiri
  • Inafaa

Je, swawm ya Ramadhaan inafuta madhambi makubwa ya mtu?

  • Ndio, hata kama hakutubia
  • Inafuta mtu akifunga mwezi mzima

Inafaa kwa mfungaji kutumia dawa ya matone kwenye masikio?

  • Asitumie matone zaidi ya matatu
  • Hapana

Inafaa kwa mfungaji kupaka wanja?

  • Ndio
  • Inafaa tu kama ni mgonjwa

Je, inafaa kwa mfungaji kupiga mbizi?

  • Ndio
  • Akizama ndani sana amefungua

Ni ipi hukumu ya aliyeingiliwa na Ramadhaan kabla ya kulipa deni la Ramadhaan iliotangulia?

  • Inafaa haina neno muhimu adhibiti idadi
  • Hapati dhambi

Ni kiasi gani cha Qur-aan kinatakiwa kusomwa katika Tarawiyh?

  • Nusu juzu
  • Hakuna kiwango maalum, ila kadri itavyorefushwa ndio bora zaidi

Ni ipi hukumu ya mfungaji kung’oa jino?

  • Akitokwa na damu nyingi amefungua
  • Inafaa

Vipi kuhusu swawm ya aliyezimia?

  • Haipo
  • Kama amepoteza fahamu kabisa hana swawm

Inafaa kwa mfungaji kutumia dawa ya matone kwenye macho?

  • Inachukiza
  • Inafaa haina neno

Joto kali na kazi ngumu inamjuzishia mtu kutofunga?

  • Ndio, ila atalipa siku nyingine
  • Hapana

Je, inafaa kwa msafiri kuendelea kula baada ya kufika katika mji wake?

  • Ndio, ila asile kushiba
  • Bora kujizuilia mpaka jua lizame

Je, kuna duaa maalum kila baada ya Rakah mbili za Tarawiyh?

  • Ipo
  • Aseme "Astaghfirullaah mara 33"

Ni lini kufunga Ramadhaan kunamuwajibikia mtoto?

  • Akifika umri wa 18
  • Anapokuwa mkubwa

Inafaa kwa mfungaji kutumia dawa ya matone kwenye pua?

  • Inafaa tu kama ameandikiwa na daktari mwaminifu
  • Ndio, japo bora ni kuepuka kwa.s pua ni njia mojawapo ya kupitisha chakula

Ni ipi hukumu ya anayepinga uwajibu wa kufunga Ramadhaan?

  • Kafiri
  • Bado ni muumini mwenye imani pungufu

Ni nani mwenye jukumu la kuwatangazia waislamu mwezi mwandamo?

  • Muislamu yeyote
  • Qaadhiy

Inafaa kumwalika chakula masikini kwa aliye na kafara ya Ramadhaan?

  • Unaweza badala yake ukamwalika chakula
  • Ni lazima ufanye yote mawili

Je, inafaa kwa aliyenuia kusafiri kuanza kula katika mji wake kabla hajaanza safari?

  • Hapana, mpaka atoke ndani ya mji wake
  • Ale tu midhali kishatia nia lakini asifanye tendo la ndoa

Je, kuna duaa maalum inayosomwa wakati wa kula daku?

  • Haipo
  • Ndio, Allaahummaa laka swumtu...