Jipime maarifa yako kuhusu ´Aqiydah sahihi
Chemsha Bongo ya ´Aqiydah sahihi 05
15:00
Nini ipi katika hizi ni moja ya maana ya kushuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah?
- Kumsifu sana
- Kumwamini kwa dhahiri
- Kujiepusha na yale aliyokataza na kukemea
Nini maana ya shirki?
- Kuamini kuwa kuna muumba mwingine asiye Allaah
- Kuamini kuwa kuna anayehukumu mwingine asiye Allaah
- Kumwabudu mungu mwengine asiye Allaah au pamoja na Allaah
Ni ipi kalima ya Tawhiyd?
- Laa ilaaha illa Allaah
- Kuswali kwa unyenyekevu
- Kuamini Mitume yote
Ni karne ngapi bora alizozisifia Mtume?
- 5
- 6
- 3; Maswahabah, wanafunzi wao na wale waliokuja baada yao
Ni ipi imani sahihi katika hizi kuhusu Malaika?
- Ni viumbe wanaokula na kunywa kama wanadamu wengine
- Ni ibara ya viumbe wasiyokuwepo kiuhalisia
- Ni viumbe wa Allaah waliyopewa majukumu mbalimbali
Je, kuna tofauti kati ya anayemwabudu Mtume na anayeabudu sanamu au jiwe?
- Ndio, anayeabudu jiwe adhabu yake ni kubwa zaidi
- Hapana, zote mbili ni shirki kubwa
- Kumwabudu Mtume sio shirki
Mtume alikuwa na miaka mingapi alipotumwa na Allaah?
- 40
- 25
- 50
Je, maneno ya Allaah ni maneno yanayosikika kwa herufi na sauti?
- Hapana, maneno kama hayo ni ya kiumbe tu
- Ni herufi lakini si kwa sauti
- Ndio, ni maneno yanayosikika kwa herufi na sauti
Je, kila kitu katika ulimwengu kinatokea baada ya matakwa ya Allaah?
- Ndio, isipokuwa tu maasi
- Ndio, mpaka maasi
- Hiyo ni imani ya kikafiri
Ni ipi hukumu ya anayepinga moja ya mambo yanayotambulika vyema katika Uislamu?
- Kafiri
- Amefanya kosa kubwa
- Kama ana mtazamo katika kupinga kwake hapati dhambi
Ni ipi hukumu ya anayeamini kuwa kitu katika dhati ya Allaah kimechanganyika na kiumbe?
- Hiyo ndio imani sahihi
- Imani hiyo ni ukafiri
- Hiyo ndio imani waliyokuwa nayo Mitume
Ni lini matendo yanakubaliwa na Allaah?
- Matendo yote yanakubaliwa maadamu mtu ana nia njema
- Matendo pekee yanayokubaliwa ni yale yaliyotimiza ikhlaasw na ufuatuaji
- Matendo ya kila muislamu mwenye imani yanakubaliwa
Ni Suurah ipi ambayo ni sawa na thuluthi ya Qur-aan?
- al-Faafiruun
- al-Ikhlaasw
- an-Naas
Je, inafaa kumtii yeyote katika kumuasi Allaah?
- Ndio, mume pekee
- Hapana, hakuna utiifu wa maasi kwa kiumbe yeyote
- Ndio, Mtume pekee
Nini ipi katika hizi ni moja ya maana ya kushuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah?
- Kumsema vizuri na kumsifu
- Kumwamini kwa dhahiri
- Kumsadikisha katika yale aliyokuja nayo
Je, ni Mtume yupi katika hawa aliyetumwa kwa watu wote?
- Ibraahiym
- Muhammad
- Aadam
Ni nini maana ya kulingana (Istiwaa) juu ya Arshi?
- Kukaa
- Kutawala
- Kuinuka na kuwa juu
Ni Suurah ipi ambayo ni sawa na robo ya Qur-aan?
- al-Baqarah
- al-Faatihah
- al-Kaafiruun
Nini ipi katika hizi ni moja ya maana ya kushuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah?
- Kumtii na kumfuata katika yale aliyokuja nayo
- Kumsema vizuri na kumsifu
- Kumwamini kwa dhahiri
Ni ipi imani sahihi juu ya Mtume Iysaa bin Maryam?
- Ameshakufa na hayuko hai
- Alizikwa kama Mitume wengine
- Alipandishwa juu mbinguni na atarudi ulimwenguni katika zama za mwisho
Kuna aina ngapi za wahy na ni zipi?
- 1; Qur-aan
- 2; Qur-aan na Sunnah Swahiyh
- 1; Sunnah Swahiyh
Je, Mtume Iysaa atarudi ulimwenguni kama Mtume au mfuasi katika wafuasi wa Mtume Muhammad?
- Atarudi kama Mtume na Shari´ah mpya
- Atarudi kama mfuasi katika wafuasi wa Mtume Muhammad
- Ameshakufa na hatorudi tena ulimwenguni