Swali: Baadhi wanasema kuwa sababu ya vijana kupungukiwa ni kule kuweka wazi mfumo na kwamba hekima inayopelekea katika kunyooka na uongofu ni kunyamaza. Unasemaje juu ya maneno haya?

Jibu: Nimeshasema kwamba kunyamaza ni kuficha haki. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِن بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ ۙ أُولَـٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّـهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ

“Hakika wale wanaoficha yale Tuliyoyateremsha katika hoja za wazi na mwongozo baada ya kuwa tumeyabainisha kwa watu ndani ya Kitabu, hao anawalaani Allaah na wanalaaniwa na kila mwenye kulaani.”[1]

Nawapongeza watu hawa kwa kupata laana kama hizi. Miongoni mwa hayo ni kwamba wanaita kunyamaza eti ni hekima. Wanaita kuwatetea Ahl-ul-Bid´ah wal-Ahwaa´ eti ni hekima. Ni vipi watu wataijua haki ilihali umenyamaza?

Fitina na shubuha zinaletwa na Ahl-ul-Bid´ah wal-Ahwaa´. Kulingania kwa Allaah, Qur-aan na kushikamana na Qur-aan na Sunnah ndio ulinganizi unaofanya ummah mzima kuwa kitu kimoja. Fitina, mipasuko na kutofautiana ni mambo yametoka kwa watu wa batili na watu wanaoeneza fitina. Wao hawanayamazi. Wanaeneza batili zao kwenye magazeti, majarida yao na darsa zao. Kisha wanataka sauti ya haki inyamaze? Wao wanaona kuwa sauti ya haki inapaswa kunyamaza na sauti za batili ndio yanatakiwa kuwa juu na kuenezwa ardhini. Je, wao wananyamaza?

Watu wa batili hawanyamazi. Hawatosheki. Hawatulii. Wana mikakati ya kijahanamu wanayoifanya. Halafu wanawataka watu wa haki wanyamaze. Allaah (´Azza wa Jall) amesema kumwambia Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

وَدُّوا لَوْ تُدْهِنُ فَيُدْهِنُونَ وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَّهِينٍ هَمَّازٍ مَّشَّاءٍ بِنَمِيمٍ مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ عُتُلٍّ بَعْدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ

”Wanatamani lau kama ungelilegeza nao pia wakalegeza na wala usimtii kila mwingi wa kuapa, mtwevu, mwingi wa kukashifu, mpitaji huku na huku akieneza uvumi, mwingi wa kuzuia ya kheri, mwenye kuvuka mipaka, mwingi wa kutenda dhambi, katili na baada ya hivyo ni mwenye kujipachika tu kabila.”[2]

Unapokuja mfumo wa Salaf wanasema kuwa unavunja na kutenganisha. Hakika si venginevyo ni kwamba matamanio na upotofu ndivo vinavyovunja na kuufarikisha ummah. Watu wa batili wanayaeneza kwa hamasa kwenye intaneti, magazeti, majarida, shule na kila mahali. Kitu ambacho ni kigumu kwao kusikia ni sauti ya haki.

[1] 2:159

[2] 68:9-13

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf-us-Sitaar, uk. 28-30
  • Imechapishwa: 09/11/2022