Pindi baba anapoona ndoa ya msichana wake ina madhara

Swali: Je, inafaa kwa walii kuzuia ndoa ya msichana wake pale anapoona kuwa ina madhara kwa mujibu wa Shari´ah?

Jibu: Ajitahidi katika jambo hilo na asimuozeshe isipokuwa kwa njia anayoona kuwa ina kheri na manufaa kwake. Wakivutana basi waende mahakamani. Lakini ni lazima kwake ajitahidi na asimuozeshe isipokuwa kwa mwanamme mwema ambaye anamstahiki mwanamke.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23837/هل-للولي-منع-زواج-المراة-لمفسدة-شرعية
  • Imechapishwa: 16/05/2024