Pesa za ribaa zinazowekwa katika akaunti

Swali: Benki huweka ribaa kwenye akaunti ya mtu. Je, inafaa kwa mtu huyo akachukua ribaa hiyo au aiache kwao?

Jibu: Aachane nayo. Ni vipi ataichukua ilihali ni ribaa?

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

 “Enyi walioamini! Mcheni Allaah na acheni yaliyobakia katika ribaa ikiwa kweli nyinyi ni waumini.[1]

Iacheni.

[1] 02:278-279

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (29)
  • Imechapishwa: 11/02/2022