Pesa iliyohifadhiwa inatakiwa kutolewa zakaah

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu ambaye anaendelea kuhifadhi pesa yake kama akiba kutoka katika mali ya mahari kwa ajili ya kuoa ambapo anaihifadhi kwa muda wa miaka kadhaa. Je, pesa hiyo inayohifadhiwa inatakiwa kutolewa zakaah?

Jibu: Ndio. Kila pesa anayohifadhi mtu inatakiwa kutolewa zakaah ijapo ameiandaa kwa ajili ya kuoa, kulipa deni, kujenga nyumba na mfano wa hayo. Pesa hiyo anatakiwa kuitolea zakaah. Zakaah inaizidisha na haiipunguzi:

خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا

“Chukua katika mali zao zakaah, uwatwaharishe na uwatakase kwazo.”  (09:103)

Zakaah ni kusafishwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4421/حكم-الزكاة-في-المال-الذي-يجمع-ويدخر
  • Imechapishwa: 17/06/2022