Pale ambapo kuapa kwa asiyekuwa Allaah inakuwa shirki kubwa

Swali: Vipi ikiwa mwapaji anamtukuza yule anayemuapia?

Jibu: Ikiwa ana imani fulani juu yake inakuwa shirki kubwa. Ikiwa ana imani kwake na anaitakidi kuwa anafaa kuabudiwa, kuombwa au yeye ni walii anayeombwa badala ya Allaah, imani hii inafanya shirki kubwa. Lakini ikiwa imemtokea mdomoni mwake pasi na kukusudia kumpenda, au akawa anamtukuza lakini haonelei kuwa anafaa kuabudiwa au imemtokea mdomoni kwa sababu ya desturi zao za zamani, katika hali hiyo inakuwa shirki ndogo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24169/حكم-من-يحلف-بغير-الله-تعظيما-او-عادة
  • Imechapishwa: 08/09/2024