Swali: Kuna mtu fakiri alinijia akaniomba pesa. Nikamwambia asubiri na nikamkusanyia pesa kutoka kwa baadhi ya watu. Nilipokuja katika miadi tuliyokubaliana hakutokozea. Je, inafaa kwangu kumpa pesa hiyo masikini mwingine?
Jibu: Ndio. Mpe masikini au wamasikini wengine.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
- Imechapishwa: 13/05/2023