Nywele zinazotoka wakati Muhrim anapiga chuku

Swali: Nywele zinazomdondoka mwenye kufanya chuku?

Jibu: Baadhi ya wanazuoni wanasema kuwa zinasamehewa, kwa sababu sio kunyoa kichwa kizima. Ni kitu kidogo tu. Baadhi ya wanazuoni wamefasiri kwa mujibu wa Hadiyth ya Ka´b na kwamba anatakiwa kutoa fidia kati ya moja katika mambo matatu:

1 – Kufunga siku tatu.

2 – Kuchinjwa kondoo.

3 – Kulisha chakula masikini sita.

Dhana yangu kubwa inanambia kuwa Ibn-ul-Qayyim (Radhiya Allaahu ´anh) amefasiri kusamehe, kwa sababu haikunakiliwa kwamba (Swalla Allâhu ´alayhi wa sallam) alitoa kafara. Kwa hiyo ikafahamisha kuwa kuumikwa kunasamehewa ile athari yake ikiwa ni kwenye nywele, kwa sababu ni kitu kidogo na sio kunyoa kichwa chote au sehemu kubwa ya kichwa. Ni kitu kidogo tu kinachonyolewa. Hata hivyo akichukua tahadhari na akatoa kafara ni jambo jema.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24058/حكم-الشعر-الذي-يسقط-عند-الحجامة-للمحرم
  • Imechapishwa: 22/08/2024