Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
وعن أنس رضي الله عنه قَالَ : مَرَّ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم بامرأةٍ تَبكي عِنْدَ قَبْرٍ، فَقَالَ : (اتّقِي الله واصْبِري) فَقَالَتْ: إِليْكَ عَنِّي؛ فإِنَّكَ لم تُصَبْ بمُصِيبَتي وَلَمْ تَعرِفْهُ، فَقيلَ لَهَا : إنَّه النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم فَأَتَتْ بَابَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم، فَلَمْ تَجِدْ عِنْدَهُ بَوَّابينَ، فقالتْ : لَمْ أعْرِفكَ، فَقَالَ : (إنَّمَا الصَّبْرُ عِنْدَ الصَّدْمَةِ الأُولى). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
.وفي رواية لمسلم: (تبكي عَلَى صَبيٍّ لَهَا)
31 – Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpitia mwanamke ambaye alikuwa analia kwenye kaburi na kumwambia: “Mche Allaah na kuwa na subira!” Akasema: “Niondokee, hujafikwa na msiba ulonifika!” [na mwanamke huyo] hakumtambua [aliyemwambia vile]. Akaambiwa: “Huyo alikuwa ni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akaenda mpaka kwenye mlango wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hakukua walinzi. Akamwambia: “Sikukutambua.” Akasema: “Hakika mambo yalivyo subira wakati wake ni pale mwanzoni mwa kupatwa na msiba.”[1]
Miongoni mwa faida za Hadiyth hii ni pamoja na kwamba mtu anapewa udhuru kutokana na ujinga alionao. Hilo linahusu ujinga juu ya hukumu ya Kishari´ah au hali. Mwanamke huyu alimwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Niondokee.”
Pamoja na kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anamwamrisha kheri na kumcha Allaah na subira. Lakini hata hivyo hakujua kuwa ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawa amempa udhuru.
[1] al-Bukhaariy na Muslim.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/228)
- Imechapishwa: 22/02/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)